Kinda wa Barcelona Ansu Fati nje kwa miezi minne kutokana na majeruhi

Pigo. Miamba ya soka la Hispania Barcelona wamekumbwa na pigo kufuatia kinda wao hatari Ansu Fati kupata majeruhi ambayo yatamfanya kuwa nje ya uwanja kwa muda wa takribani miezi minne. Ansu Fati mwenye umri wa miaka 18 ambaye kwa msimu huu 2020/21 alikuwa kwenye kiwango bora amefanyiwa salama upasuaji wa goti lake la upande wa kushoto baada ya kuumia katika mchezo wa Ligi dhidi ya Real Betis.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Hispania alifanyiwa mabadiliko katika mchezo huo ambao uliisha kwa Barca kushinda 5-2 siku ya Jumamosi. Fati amecheza mechi 10 na kufunga goli tano na kutoa asisti mbili kwa msimu huu pekee katika umri wa miaka kumi na nane.

Author: Asifiwe Mbembela