Kipa Buffon aamua kuzitundika glovu

Klabu ya PSG imetoa taarifa kuwa itaachana na mlinda mlango Gianluigi Buffon pindi mkataba wake utakapo malizika siku za usoni.
 
Mlinda mlango huyo wa Kiitaliano alijiunga na matajiri wa Ufaransa msimu wa mwaka jana kama mchezaji huru akitokea Juventus.
 
Buffon, 41, amecheza michezo 25 katika mashindano yote ambapo kikosi cha kocha Thomas Tuchel kikifanikiwa kubeba ubingwa wa Ligue 1 na kupoteza nafasi ya kutwaa mataji mengine matatu. Na sasa klabu imethibitisha kutomuongeza mkataba mlinda mlango huyo.
 
“Kufuatia mazungumzo yetu(Paris Saint-Germain) na Gianluigi Buffon tumeafikiana kutompa mkataba mwingine mkongwe huyo.” Mkataba wa kuitumikia PSG kwa Buffon unafikia ukomo Juni 30, 2019.

Author: Bruce Amani