Kipa wa Cameroon Onana apunguziwa adhabu ya matumizi ya madawa

Mlinda mlango wa Ajax ya Uholanzi na Timu ya Taifa ya Cameroon Andrea Onana amepunguziwa adhabu ya makosa ya matumizi ya madawa yaliyopigwa marufuku michezoni mpaka miezi tisa kufuatia rufaa yake kwa Mahakama ya Usuluhishi Michezoni (CAS).
Kipa huyo mwenye umri wa miaka 25, alifungiwa mwezi wa pili kwa adhabu ya miezi 12 na Bodi ya Shirikisho la Kandanda barani Ulaya Uefa.
Onana alikutwa na hatia ya matumizi ya madawa hayo baada ya kuchukuliwa sampuli ya mkojo katika uchunguzi maalumu ulioanzishwa Octoba 30, mwaka Jana kufuatia timu hiyo kuondolewa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Katika utetezi wake, kipa huyo alieleza kuwa alitumia dawa kwa bahati mbaya akidhania ni dawa za kutuliza maumivu za aspirin, ambapo aliomba kupunguziwa adhabu.
Maamuzi hayo ya CAS yanamaanisha kuwa kifungo cha kipa huyo kitafikia tamati Novemba 4 hivyo atakoaa mechi za ufunguzi wa mechi ya Ligi Kuu nchini Uholanzi za klabu ya Ajax lakini atakuwepo kwenye mechi za Cameroon za Kombe la Mataifa Bingwa Afrika Afcon mwezi Januari 2022.

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares