Kipa wa Everton Jordan Pickford akwepa rungu ya FA kutokana tukio la van Dijk

Mlinda mlango wa Everton Jordan Pickford hatakutana na rungu la FA kwa kumfanyia faulo mbaya mlinzi wa kati wa Liverpool Virgil van Dijk katika mechi ya dabi ya Jiji la Merseyside Jumamosi iliyopita. Chama cha Soka England kimelirudia tukio la faulo hiyo kwa kuwaulizia waamuzi na wasimamizi wa VAR. Beki huyo wa Liverpool alipata majeruhi ya goti ambayo huenda akawa nje kwa muda mrefu wa takribani miezi sita hadi minane.

Licha ya kurudia maamuzi ya waamuzi kwenye mchezo huo, FA ina mamlaka madogo ya kuamua tofauti na kile walichokiona waamuzi, ambapo baada ya kutazama wamebaina kuwa changamoto ya kimichezo.

Author: Bruce Amani