Kipchoge agombea Tuzo ya IAAF ya Mwanariadha Bora Mwanamme

Eliud Kipchoge ni miongoni mwa wanariadha watano wanaowania tuzo ya Mwanariadha Bora Mwanamme wa mwaka wa 2019

Mkenya huyo mwenye umri wa miaka 35, alikuwa mwanariadha wa kwanza kukimbia mbio za marathon chini ya saa mbili katika jaribio lake la Ineos 1:59 Challenge mjini Vienna, Austria mwezi Oktoba.

Kipchoge pia aliweka rekodi ya mbio za London Marathon kwa kutumia muda wa saa mbili, dakika mbili na sekunde 37 mapema mwaka huu.

Wamarekani Sam Kendricks na Noah Lyles, Mganda Joshua Cheptegei  na Mnorway Karsten Warholm pia wanawania tuzo hiyo.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends