Kipchoge Ajipanga Kufanya Makubwa Berlin Marathon

88

Mfukuza upepo wa kimataifa wa Kenya Eliud Kipchoge amesema ameanza maandalizi ya mashindano ya mbio za Berlin Marathon ambayo yamepangwa Septamba 25, 2022.

Mshindi huyo mara mbili wa Olimpiki anayeshikilia rekodi ya dunia amesema kwa maandalizi ambayo anaendelea kuyafanya bila shaka ataendelea kufanya vizuri kwenye Marathon ambayo inafanyika Berlin ikiwa ni mara yake ya nne kushiriki.

Kipchoge mwenye umri wa miaka 37, akiwa anashika rekodi ya kukimbia Marathon chini ya masaa mawili anasema lengo lake ni kukimbia kwa muda mfupi zaidi ili kuendelea kuweka rekodi zake sawa.

“Naamini bado naweza kufanya vizuri hapa Berlin, kama nitashindwa kuweka rekodi ya kidunia angalau kuweka rekodi ya mashindano husika. Sijui itakuwa rekodi gani lakini itakuja tu”, alisema Kipchoge mmoja ya wakimbiaji walioweka heshima ya riadha nchini Kenya.

Moja ya washindani wa karibu ambao Kipchoge atakuwa anashindana nao ni mshindi wa Marathon iliyopita raia wa Ethiopia Guye Adola, Kenenisa Bekele na Bethwell Ywgon.

Author: Bruce Amani