Kipchoge aweka historia katika marathon

Eliud Kipchoge amekuwa mtu wa kwanza katika historia ya mbio za marathon kukimbia kilomita 42 kwa muda wa chini ya saa mbili

Raia huyo wa Kenya alikimbia umbali wa kilomita 42.2 katika saa moja dakika 59 na sekunde 40 katika jaribio la Ineos Challenge 159 mjini Vienna nchini Austria siku ya Jumamosi.

Haitatambulika kuwa rekodi mpya ya dunia katika mbio hizo kwa kuwa halikuwa shindano la kila mtu mbali na kwamba alitumia kundi la wanariadha wa kudhibiti kasi waliokuwa wakishirikiana naye na kutoka.

Bingwa huyo wa Olimpiki alikuwa ameikosa rekodi hiyo na sekunde 25 katika jaribio lake la hapo awali 2017.

Alipogundua kwamba alikuwa anakaribia kuweka historia , wanariadha waliokuwa wakidhibiti kasi ya mbio hizo walirudi nyuma na kumwacha bingwa huyo kutimka hadi katika utepe huku akishangiliwa na mashabiki wengi mji mkuu wa Austria.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends