Kipsang afungiwa mashindano ya riadha katika kesi ya doping

Bingwa mara mbili wa mbio za London Marathon Mkenya Wilson Kipsang amefungiwa kushiriki shindano lolote la riadha kufuatia na kuingilia uchunguzi wa madai ya kutumia dawa zilizopigwa marufuku michezoni.

Wakuu wa riadha duniani wanasema Kipsang hatashiriki shindano lolote mpaka shauri lake litakaposikilizwa.

Kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa na WADA, mwanariadha anapaswa kutoa ushirikiano madhubuti wakati wote wa mchakato wa kuchunguza ikiwa alitumia dawa zilizokatazwa michezoni.

Mataifa kadhaa duniani wanariadha wake wamefungiwa kushiriki mashindano yoyote baada ya serikali ama mamlaka za nchi zao kubainika kutotoa ushirikiano wakati wa mchakato wa uchunguzi huku Urusi ikipigwa marufuku kushiriki michuano ya Olimpiki itakayofanyika Tokyo nchini Japan.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends