Kitasa wa Azam aramba mkataba mpya

202

Mlinzi wa kati wa Azam FC na timu ya taifa ya Ghana Daniel Amoah, ameongeza kandarasi mpya ya kuendelea kukitumikia kikosi hicho.

Nyota huyo wa zamani wa Medeama, ameingia Mkataba wa miaka miwili na sasa kandarasi hiyo itamalizika Novemba 2024.
Amoah ambaye alifika nchini Tanzania miaka mitano iliyopita, amesaini mkataba huo mbele ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Amin ‘Popat’.

Author: Asifiwe Mbembela