Klopp amumwagia sifa Ralf Rangnick wa Man United

26

Kocha wa kikosi cha Majogoo wa Jiji la Merseyside Liverpool Jurgen Klopp amemsifia kocha mtarajiwa wa Manchester United Ralf Rangnick kuwa ni kocha mzuri kiasi kwamba siyo taarifa nzuri kwa baadhi ya timu.

“Katika hali ya kushangaza Mwalimu mwingine mzuri anakuja kwenye Ligi Kuu England”.

Klopp amesema hayo wakati anazungumzia maandalizi ya kikosi chake kuelekea mtanange wa wikiendi hii wa Ligi Kuu dhidi ya Southamption Anfield, ambapo kutajwa wa Ralf Rangnick amekuelezea kuwa kunaweza kwenda kufufua upinzani baina ya Liverpool na Manchester United, Klopp na Rangnick.

Wote wakiwa ni raia wa Ujerumani, lakini Klopp ni Mwanafunzi wa Rangnick miaka ya 1999, 2000, kwa sasa kocha huyo mwenye taaluma ya Ukurugenzi wa Ufundi anahudumu katika nafasi hiyo pale Lokomotiv Moscow.

Rangnick mwenye umri wa miaka 63, amewai kupitia Ujerumani katika klabu mbalimbali mathalani RB Leipzig, Hoffenheim, Stuttgart, Schalke 04 na Hannover ambapo mara kadhaa walichuana na Klopp enzi hizo na yeye akiwa Mainz na Borrusia Dortmund.

“United wataonekana kama timu kwa sasa (muunganiko)”, alisema Klopp, 54.

“Ni kocha mzuri kweli, mwenye uzoefu mkubwa na soka, ambapo alivijenga vilabu ambavyo havikuwa na majina (Hoffenheim na RB Leipzig) kuwa vikubwa na tishio”.

United bado haijamtambulisha rasmi Rangnick kuwa kocha wao wa muda kurithi mikoba ya Ole Gunnar Solskjaer lakini mazungumzo baina ya pande mbili yamekamilika kilichobakia ni klabu yake ya sasa kuridhia.

Hata hivyo, imeelezwa kuwa kocha huyo anaweza kutambulishwa baada ya mchezo wa Jumapili ambao United watakuwa ugenini Stamford Bridge kumenyana na Chelsea, kocha akiwa ni Michael Carrick.

Author: Bruce Amani