Klopp awatisha Atletico licha ya kushindwa

Jurgen Klopp amewaonya Atletico Madrid kuwa wasishangilie kuibuka na ushindi wa mchezo wa raundi ya kwanza ya Uefa champions league kana kwamba wameshacheza Anfield mkondo wa pili.

Klopp amesema tumecheza kipindi kimoja Madrid bado dakika nyingine 45 za kipindi cha pili hivyo Atletico Madrid hawapaswi kuwa na furaha kiasi hicho.

Kauli ya Klopp inakuja siku moja baada ya kikosi chake kukubali kichapo cha goli 1-0 dhidi ya Atletico ya Someone katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya mkondo wa kwanza wa hatua ya 16 bora uliopigwa dimba la Wanda Mopolitano.

Goli pekee lililoamua mtanange huo lilifungwa na  Saul Niguez na kuipa ushindi dhidi ya Mabingwa Ulaya watetei.

“Mashabiki wa Atletico ambao mtaweza kununua tiketi, karibu Anfield”, alisema Klopp.

“Tunazungumza kuhusu kipindi kimoja cha mchezo, lakini pia tunazungumza kuhusu nguvu ya uwanja wetu, hakuna mwenye kupinga kuhusu nguvu yetu linalokuka suala la Anfield. Kila shabiki anakuwa na hamasa hali kadhalika kwa wachezaji, Hakika watapata hisi uchungu kucheza dakika nyingine 45 uwanjani kwetu”

Liverpool hawakuweza kulenga lango hata mara moja ikiwa na mara ya pili wanashindwa kulenga lango kwa shuti katika mchezo tangu mwaka 2015.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends