KMC yapunguzwa kasi katika ligi kuu ya Tanzania

Ligi kuu Tanzania bara imeendelea leo Ijumaa kwa michezo minne iliyochezwa katika viwanja tofauti ambapo ligi hiyo ikiwa ni mzunguko wa pili wa michuano hiyo.

Katika mchezo wa Mabatini mkoani Pwani Ruvu Shooting imeibamiza klabu ya Kizazi kipya Mbeya City kwa goli 1-0 bila, goli lililofungwa na Patrick Bwire.

Msemaji wa Ruvu Shooting amesema “Moto wa kufanya vizuri hautazimwa na tutaendelea na Papaswa Squared mpaka kwa Coastal Union” alisema Masau ambaye mbali na kuwa Msemaji wa Ruvu pia ni Mwalimu wa Shule ya Msingi Makumbusho.

Mtanange wa pili ni ule uliofanyika katika uwanja wa Kaitaba Mkoani Kagera ambapo Kagera Sugar walikuwa wenyeji wa Tanzania Prison, mchezo umemalizika kwa TP kuibuka na ushindi wa goli 2-0. Tanzania Prison imefikisha alama 20 katika nafasi ya 17.

Wakati huo huo JKT Tanzania imeibuka na ushindi wa goli 3-0 dhidi ya Mwadui FC katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Mwadui Complex, baada ya matokeo hayo JKT Tanzania ina alama 29 katika nafasi ya 8 ya msimamo wa TPL.

KMC ambayo ilikuwa katika kiwango bora katika michezo mitano iliyofanyika Uwanja wa Uhuru imelazimisha sare na Stand United katika Uwanja wa Kambarage Shinyanga. Baada ya matokeo hayo KMC itaendelea kushikilia nafasi ya tatu ya ligi kuu Tanzania bara.

Yanga inaendelea kuongoza ligi kwa alama 53, Azam nafasi ya tatu alama 47, KMC nafasi ya tatu na 35 na Simba pamoja na timu nyingine. Mshindi wa ligi ya kandanda ataibuka na taji sambamba na kuiwakilishi nchi Ligi ya Mabingwa Afrika.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends