Kocha Garcia asaini mkataba mpya na Marseille

Klabu ya Olympique Marseille imewapa mikataba mipya kocha Rudi Garcia na mkurugenzi wa spoti Andoni Zubizarreta. Garcia na Zubizarreya wamesaini mikataba mipya inayowaweka katika klabu hiyo hadi mwaka wa 2021.

Garcia alijiunga na Marseille mwaka wa 2016 baada ya kuzifunza Roma na Lille ambapo ni pamoja na taji la Ligi kuu ya Ufaransa Ligue 1 katika msimu wa 2010-11 na Lille na akamaliza katika nafasi ya pili kwenye Serie A na klabu ya Roma.

Kocha huyo aliifikisha Marseille katika fainali ya Europa League msimu uliopita, ijapokuwa timu yake ilizabwa vibaya sana na Atletico Madrid 3-0.

Zubizarreta, kipa wa zamani wa Uhispania, awali alikuwa katika uongozi wa Athletic Bilbao na FC Barcelona kabla ya kujiunga na Marseille.

Kwenye ligi, wako katika nafasi ya tano na pointi 19, ikiwa ni pengo la pointi 11 nyuma ya viongozi Paris Saint-Germain.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends