Kocha Koeman atetea kushuka kwa kiwango cha Lionel Messi

104

Kocha mkuu wa FC Barcelona Ronald Koeman ametetea kiwango cha staa wa kikosi cha Barca Lionel Messi kuwa kitarudi katika hali tuliyozoea. Koeman amesema hayo huku kukiwa na maneno kuwa Messi hana furaha ndani ya Camp Nou tangu alipolazimisha uhamisho wa kuondoka klabuni hapo ambapo sababu kubwa ni usajili mbovu ndani ya timu hiyo.

Fowadi huyo raia wa Argentina amefunga goli moja pekee msimu huu. “Sina hofu yoyote katika kiwango na juhudi zake,”. Alisema Koeman ambaye kikosi chake kitacheza mechi ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya leo Jumanne dhidi ya Ferencvaros.

“Wakati kama huu unaweza kurudisha makali yake. Kunapokuwa na mechi za hapa na pale (mashindano tofauti tofauti humfanya mchezaji kufikiria kuhusu michezo tu”. Messi yuko kwenye mwaka wa mwisho kwenye mkataba wake ambapo katika michuano ya Ulaya atakutana na mshindani wake wa muda mrefu Cristiano Ronaldo ambaye wako kundi moja la G mashindano ambayo Messi alishinda mwaka 2015.

Miamba ya soka la Italia Juventus watakutana dhidi ya Barcelona ambayo ina kocha mpya Ronald Koeman ambaye anategemea kumpa taji hilo staa na nahodha wa kikosi hicho Lionel Messi.

Author: Bruce Amani