Kocha Loew aridhishwa na kufufuka kwa timu ya taifa ya Ujerumani

Kocha wa timu ya taifa ya Ujeurmani Joachim Loew amesema  kufufuka kwa  timu  ya  taifa  kumekuwa  hatua  nzuri  sana, baada ya  kuondolewa  katika  hali  ya  kukatisha  tamaa  na  kwa  fedhaha katika  fainali  za  kombe  la  dunia  mwaka  2018  nchini  Urusi.

Katika  mahojiano  na  gazeti  la  michezo  la Kicker, Loew  alikiri  kwamba  hakuona mapungufu yaliyopo yataathiri utendaji  wa  timu  yake baada  ya  miezi 12  iliyopita  kushuhudia awamu  ya  kufuzu iliyokuwa sahihi  kabisa pamoja  na  iúbingwa  wa  kombe  la  shirikisho, Confederation.

Baada ya  kombe  la  dunia alitarajia wachezaji kuamka  katika  ligi  ya  mataifa, lakini  baada  ya  kipigo cha  mabao 3-0 dhidi  ya  Uholanzi  mwezi  Oktoba  alitanabahi  kwamba  “muda  sasa  umewadia  wa  mabadiliko”.

Author: Bruce Amani