Kocha Tuchel alalamikia VAR, tulitakiwa kushinda mbele ya Leicester City

Kocha wa Chelsea Thomas Tuchel amesema timu yake ilifanya kila linalowezekana lakini maamuzi ya Video Saidizi kwa Waamuzi VAR yaliwaumiza na kuwanyima ushindi katika mechi ya Kombe la FA dhidi ya Leicester City uliopigwa dimba la Wembley Jumamosi.
The Blues walikutana na kichapo cha goli 1-0 kutoka kwa Leicester City kufuatia goli bora la kiungo mshambuliaji wa Ubeligiji Youri Tielemans na kuinyima Chelsea uwezekano wa kuondoka na mataji mawili msimu huu.
Tuchel anayesema hayo akizungumzia tukio la mchezaji wa Leicester Ayoze Perez kuonekana kunawa mpira eneo la hatari lakini baada ya mapitio ya VAR ilionyesha haikuwa kusudi lake (mpira ulifuata mkono).
“Wachezaji walisema mpira ulienda moja kwa moja mkononi” alisema Tuchel ambaye ni kocha wa zamani wa Paris St-Germain ya Ufaransa.
“Unakuwa mchezo wa pili kwa kuumizwa na maamuzi kama hayo, VAR inatuumiza, utakumbuka mechi ya Arsenal pia ilitokea hivi”.
“Sio mtaalamu wa kutafsiri sheria ya huu kuwa mpira ulifuata mkono au mkono ulifuata mpira”
Chelsea pia walikuwa kwenye nafasi ya kupata goli baada ya mlinzi wa kushoto Ben Chilwell kukwamisha mpira nyavuni lakini ilionekana kuwa alikuwa kwenye eneo la kuotea.
Hata hivyo, licha ya matokeo hayo lakini kocha Tuchel amesema amefurahia namna vijana wake walivyopambana.

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares