Kocha wa Arsenal Arteta amepona kabisa virusi vya corona

Kocha wa Arsenal Mikel Arteta anasema kuwa ”amepona kabisa” virusi vya corona. Mhispania huyo mwenye umri wa miaka 37, alikuwa mkufunzi wa kwanza wa ligi ya Premier kupatikana na virusi vya corona Machi 13.

Aliripotiwa kujihisi vibaya baada ya kuwa karibu na Evangelos Marinakis – mmiliki wa klabu ya Ugiriki ya Olympiakos, aliyekuwa amehibitishwa kuwa na ugonjwa huo, wakati timu yake ilicheza na Arsenal katika ligi ya Europa Februari – na kupatikana na coronavirus Machi 10.

Arteta anasema: “Iilimchukua siku tatu hadi nne kuanza kujihisi vyema, nikiwa na nguvu, nazo dalili zikapotea.”

Akizungumza na kituo cha televisheni cha Uhispania La Sexta aliongeza kusema: “Najihisi vyema sasa. Nahisi nimepona.”

Wachezaji wa Gunners walitarajiwa kurejea uwanjani kwa mazoezi sikiu ya Jumanne baada ya kukamilisha siku 14 ya kujitenga ilipobainika Arteta ameambukizwa virusi vya corona lakini mpango huo umeahirishwa.

“Kutokana na hali ilivyo sasa, tunafahamu itakuwa utepetevu mkubwa kuwaambia wachezaji warudi uwanjani wakati huu,” ilisema taarifa kutoka kwa usimamizi kwa klabu hiyo ya London kaskazini.

Author: Bruce Amani

Facebook Comments