Kocha wa Chelsea Tuchel amwaga sifa kwa Mason Mount

Kocha wa Chelsea Thomas Tuchel amesema kiungo mshambuliaji wa klabu hiyo Mason Mount amepiga hatua kubwa katika namna ambavyo anacheza, baada ya kiungo huyo kufunga goli moja kwenye ushindi wa goli 2-0 dhidi ya FC Porto Ligi ya Mabingwa Ulaya mkondo wa kwanza robo fainali.

Mount aliweka Chelsea kifua mbele baada ya kufunga goli la kwanza akimalizia pasi ya Jorginho kabla ya beki wa pembeni Ben Chilwell kukamilisha hesabu za The Blues mkondo wa kwanza.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa England mwenye umri wa miaka 22, amefikisha bao tatu katika mechi nne zilizopita.

“Umaliziaji wa bao ulikuwa bora sana, ameimarika katika uchezaji maradufu”, alisema Tuchel baada ya mcheo huo.

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares