Kocha wa Gladbach Marco Rose asema hatoondoka na wachezaji nyota kuelekea Dortmund

Kocha wa Borussia Moenchengladbach Marco Rose ameahidi kutochukua wachezaji nyota wowote wa Gladbach anapoelekea kuinoa Borussia Dortmund msimu ujao. Siku ya Jumatatu siri kubwa iliwekwa wazi, Kocha wa Gladbach Marco Rose ataondoka na kujiunga Dortmund msimu ujao.

“Niliamua kuchukua kazi hiyo ya kusisimua katika Borussia Dortmund. Haikuwa rahisi,” amesema Rose katika mkutano na waandishi wa habari. Kocha Rose mwenye umri wa miaka 44 ameifikisha Gladbach kwenye hatua ya mchujo katika Ligi ya Mabingwa Ulaya ambapo watachuana na Manchester City siku ya Jumatano ya tarehe 24.2.2021 katika mchezo wao wa raundi ya 16 utakayo fanyika Budapest.

Chini ya usimamizi wake, Gladbach ameshinda mechi dhidi ya vilabu vya juu vya Bundesliga kama vile Bayern Munich, RB Leipzig na Dortmund nyumbani msimu huu huko Borussia Park na kutoka sare na Real Madrid katika michuano ya Ligi ya Mabingwa.

Wachezaji kama mshambuliaji Marcus Thuram na kiungo wa kati Florian Neuhaus chini ya ukufunzi wake Rose wamefanikiwa kuitwa kujiunga na timu ya taifa ya wanalowakilisha. Wakati anaondoka Salzburg mnamo 2019, aliwachukua beki wa kulia Stefan Lainer na kiungo wa kati Hannes Wolf kutoka klabu hio ya Austria hadi Gladbach.

Alipoulizwa kama historia itajirudia atakapojiunga na Dortmund Rose amesema, “Ikiwa nimesema sitachukua mchezaji kwenda naye Dortmund, basi sitampeleka mchezaji Dortmund. Nimemaliza.”

Borrusia Moenchengladbach italazimika kutafuta benchi la ukufunzi zima kwa sababu Rose anaondoka na wasaidizi wake wote watatu kuelekea Dortmund. Lakini kwa sasa anashikilia kuwa ataendelea kuinoa Gladbach kwa ari kuelekea mechi kati ya Gladbach na Doermund ya kuwania Kombe la Ujerumani mnamo Machi 2.

“Hakuna kilichobadilika katika mtazamo wangu kwa mwajiri wangu, bado ni chanya. Ninahusika kwa asilimia 100,” amesisistiza Rose. Katika jedwali la Bundesliga, Gladbach na Dortmund zote zina jumla ya pointi 33, pointi sita kabla ya kuvuzu kwa michuano ya Magingwa.

Taarifa za kuondoka kwake zimewkasirisha mashabiki wa Gladbach na kukiwekwa mabango ya kumkejeli Rose nje ya uwanja wa mazoezi wa klabu hio. Kocha Jesse March, anayesimamia sasa Red Bull Salzburg na Florian Kohfeldt wa Werder Bremen ni miongoni mwa wanaoweza kuchukua nafasi ya Rose huko Gladbach.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares