Kocha wa Gor aangazia macho KPL baada ya kufurushwa CAF

46

Kocha wa Gor Mahia Steve Polack anadai licha ya kunyukwa na DC Motema Pembe ya DRC siku ya Jumapili katika mechi ya mchujo ya CAF, wana imani kuwa watatetea taji lao la KPL.

KO’gallo ambao wamefuzu kwa awamu ya makundi vipindi viwili vilivyopita walipoteza 2-1 na kubanduliwa baada ya kushindwa kwa jumla ya mabao 3-2 mjini Kisnhasa. KO’galo walirejea nchini jana na wameanza mazoezi tayari kwa mchuano wa kukata na shoka dhidi ya AFC Leopeards Jumapili hii.

Author: Bruce Amani