Kocha wa Kihispania afariki dunia kutonana na virusi vya corona

Meneja wa klabu ya vijana wa Atletico Portada Alta ya Hispania Francisco Garcia amefariki dunia kutokana na Virusi Corona akiwa bado mdogo umri wa miaka 21.
Garcia alikuwa akifanya kazi na timu ya watoto ya Atletico Portada Alta iliyopo Malaga tangu mwaka 2016, lakini baada ya vipimo ilibainika kuwa alikuwa na ugonjwa wa saratani ya damu uliosababisha mwili wake kukosa kinga za kupambana na virusi vya corona baada ya kupelekwa hospitalini.
Zaidi ya watu 300 tayari imesharipotiwa kuwa wamefariki nchini Hispania tangu kuzuka kwa virusi vya corona Covid-19.
Garcia alikuwa mwathirika wa tano wa janga hilo katika mkoa wa Malaga nchini Hispania, lakini kwa sasa inaelezwa ndiye muathirika mdogo zaidi aliyepata virusi hivyo katika mkoa huo huku waathirika wengi wakiwa watu wenye umri wa miaka 70 au 80.
Baada ya kufika hospitalini, wataalamu walimkuta Mwalimu huyo akiwa anaugua ugonjwa wa saratani ya damu uliosababisha mwili kushindwa kupambana na virusi vya corona.
Inaelezwa kuwa Garcia anaweza kuwa mtu mdogo kabisa ulimwenguni kufa kwa sababu ya ugonjwa wa corona ingawa yupo mtoto anayedaiwa pia kuugua virusi vya Corona.
Shughuli za soka nchini Hispania, pamoja na ligi ya La Liga, tayari imesimamishwa kwa nia ya kulinda wachezaji na kuzuia kuenea kwa virusi vya corona.

Author: Bruce Amani

Facebook Comments