Kocha wa Milan Gattuso ahofia kazi yake

Kocha wa AC Milan Gennaro Gattuso amekiri kibarua chake kipo kuchunguzwa baada ya timu hiyo kufanya vibaya katika mchezo wa Europa ligi dhidi ya Real Betis.

Milan inashika nafasi ya 12 katika msimamo wa Seria A ambapo ilifungwa dhidi ya wapinzani wao Inter Milan ikifuatiwa na kipigo kingine dhidi ya timu kutoka Hispania Real Betis kwenye usiku wa Europa.

Akizungumza na Wanahabari Gattuso amesema ‘Ni kweli kibarua changu kinajadiliwa na kuchunguzwa

Huwa ni vigumu kocha kupata usingizi pale timu yake  inapocheza vibaya kama hivi’ alisema Gattuso, 40.

Gattuso, ambaye amewai kuwa kiungo wa Milan na Italia alichukua fursa ya kuwa kocha tangu Novemba  2017 ambapo sasa imekuwa miaka 7 tangu mara ya mwisho kubeba ndoo ya ubingwa.

Gazeti la La Gazzetta Dello Sport la Italia limethibitisha kuwa kibarua ya Gattuso kipo salama mpaka sasa ingawa michezo mitatu iliyombele ya timu hiyo ni muhimu kushinda kuliko kitu chochote kile.

‘Ninahofu, nimekatishwa tamaa nina chuki pia hasa ya mimi mwenyewe,’ alisema sifikiria kuhusu hali yangu, nafikiria namna bora ya kurekebisha tatizo hili linalotukabili’

“Mimi ndio mtu wa kwanza kuulizwa kuhusu hili, yote ni kwa sababu yangu, naifundisha klabu kubwa hivyo ni wajibu kwangu kuwajibika na hali inayoendelea hivi sasa’

Sasa nahitaji kujua ni yupi yupo katika hali ya akili nzuri”, Mda mwingine tumekuwa tunatumia mbinu ambazo hata hatukuzifanyia mazoezi wala kujiandaa, Tuna hofu kubwa ya kufanya makosa kuliko kitu chochote hivi sasa ndani ya timu’

Mfumo wa namna tunavyocheza hauchangia kabisa, Milan imepoteza utambulisho wake” namna tunavyocheza inanichanganya kwa kweli, inawezekana  kabisa kuwa mimi na  viongozi wangu hatuelewi na haturidhishwi na mfumo huu, hatuwezi kuelezea kiwango hiki, kufungwa hakutuumizi Zaidi ya kiwango kibovu cha timu yangu.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends