Kocha wa Munich Flick ajigamba kufanya vizuri mbele ya Lazio katika Ligi ya Mabingwa

Kocha Mkuu wa Bayern Munich Hansi Flick amesema kuwa ni lazima timu yake itarudi katika ubora kwenye mechi dhidi ya Lazio mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya 16 bora utakaopigwa kesho Jumanne.

Bayern washindi wa mataji sita ndani ya miezi tisa waliangusha alama zote tatu katika mchezo wa Ligi Kuu nchini Ujerumani Bundesliga wikiendi hii ikiwa ni siku chache baada ya kushinda Kombe la Dunia ngazi ya vilabu.

Kocha Flick atakosa huduma ya nyota wake Corentin Tolisso, ambaye ni majeruhi na Thomas Muller, ambaye anajitenga mwenyewe kutokana na kuwa dalili za Covid-19.

“Hautakuwa mchezo rahisi hata kidogo, lakini lazima tupambane”, alisema kocha Flick.

Itakuwa mara ya kwanza kwa timu ya Lazio kucheza mechi na Bayern Munich kwenye mechi za mashindano ingawa timu za Italia zimekuwa wateja wa vilabu vya Ujerumani.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares