Kocha wa Namungo ana matumaini kibao kuwavaa Nkana FC Kombe la Shirikisho

Kocha wa Namungo FC Hemed Morocco amesema anaamini kikosi cha timu yake kinaweza kushinda dhidi ya Nkana FC katika mchezo wa Kombe la Shirikisho barani Afrika hatua ya makundi mchezo wa tatu utakaopigwa kwa Mkapa Jumapili.

Kukiwa na ruhusa ya kuingiza mashabiki elfu 10,000 baada ya Shirikisho la Kandanda Afrika – CAF kulegeza vizuizi nchini Tanzania, Namungo watakuwa kwenye kibarua cha kutafuta ushindi wa kwanza katika hatua hiyo ya makundi kufuatia kupoteza mechi mbili za awali.

Kocha Morocco amesema hayo wakati akiuzungumzia mchezo huo kuwa wachezaji wake hawana uzoefu na mashindano hayo kama ilivyo kwa Nkana lakini anaamini wakifuata maelekezo yake wanaweza kuvuna ushindi hasa wanapocheza nyumbani (uwanja wa Mkapa).

Nkana FC inayoshiriki Ligi Kuu ya Zambia, inashika mkia wakati Namungo inashika nafasi ya tatu zote zikiwa hazina alama hata moja katika mechi mbili, kinara wa kundi ni Pyramid Fc ya Misri na Raja Casablanca.

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares