Kocha wa PSG Pochettino akutwa na maambukizi ya Covid-19

Kocha wa Paris St-Germain Mauricio Pochettino amekutwa na dalili za maambukizi ya virusi vya Corona ambapo sasa atakosa mechi mbili za timu hiyo.

Kocha huyo wa zamani wa Tottenham, 48, amekuwa katika nafasi ya ukocha ndani ya PSG mwanzoni mwa mwezi Januari na tayari ameshinda taji moja katika mechi tatu ambazo amekinoa kikosi cha matajiri hao wa Jiji la Paris baada ya kuifunga Marseille goli 2-1 na kutwaa Trophees des champion.

PGS watakutana na Angers Jumapili katika mechi ya Ligi Kuu nchini humo na Montpellier Ijumaa ya Januari 22.

Taarifa ya klabu ilisema kuwa Pochettino atatakiwa kujitenga mwenyewe kufuata utaratibu uliowekwa na taifa.

Timu hiyo kwa sasa itakuwa chini ya kocha msaidizi Jesus Perez na Miguel D’Agostino.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares