Kocha wa Sofapaka John Baraza asema wana uwezo wa kushinda ligi

Hata baada ya kutofuzu kushiriki michuano ya bara Afrika, klabu ya Sofapaka nchini Kenya bado ina uwezo mkubwa wa kushinda ligi ya Kenya msimu ujao. Hayo ni matamshi ya kocha wa klabu hio John Baraza.

Baraza anasema japo hatarajii kuwapoteza wachezaji wengi wakutegemewa, analenga kuboresha kikosi chake kabla ya msimu ujao kuanza.

Anasema analenga kuimarisha safu ya ulinzi akiongeza kuwa walifungwa mabao mengi mno msimu uliopita. Sofapaka walofungwa kwenye faianali ya kuwania kombe La Shield na Kariobangi Sharks, walimaliza katika nafasi ya tano kwenye ligi ya Kenya iliotwaliwa na Gor Mahia.

Mara ya mwisho na ya kwanza kwao kulitwaa taji la Kenya ilikua mwaka wa 2009 walipojiunga na ligi ya Kenya – KPL

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends