Kocha wa Ujerumani Loew akiri makosa

Kocha  wa  timu  ya  taifa  ya  Ujerumani Joachim Loew amekiri kufanya  makosa  kadhaa  ambayo  yalichangia  katika hali  mbaya iliyojitokeza katika kombe la  dunia lakini ameamua  kuchukua  hatua  chache  za  kufanya  mabadiliko  katika  kikosi chake kitakachoshiriki  katika michezo ya  kimataifa mwezi  ujao, akisema, akisema  mlingano  wa  uzoefu  na  vijana ni  muhimu.

Loew amesema Ujerumani, ambayo ilitolewa  mapema  katika  kombe  la  dunia  kwa  mara  ya  kwanza  katika  muda  wa  miaka  80 katika awamu  ya  makundi, haikupaswa kucheza mchezo  wao  wa kawaida  wa  kumiliki  wa  mchezo  katika  mashindano  hayo  ya  mtoano wakati  timu  zilikuwa  zkifanya  mashambulizi  ya  ghafla  kwa  mafanikio  makubwa.

Pia  amesema alishindwa kuingiza hali ya kuona umuhimu na hisia  miongoni mwa wachezaji wake ambao  walipoteza  michezo yao miwili  kati  ya  mitatu  katika  awamu ya  makundi. Miongoni mwa  wachezaji  aliowaita  katika  kikosi  cha  Ujerumani katika michezo  ya  ligi  ya  mataifa  dhidi  ya  Ufaransa  Septemba  6  na   mchezo  wa  kirafiki  dhidi  ya  Peru  siku  tatu  baadaye, ni  wachezaji  wanaorejea  katika  kikosi  hicho Leroy Sane, Nils  Petersen  na  jonathan Tah  pamoja  na  wageni  Kai Havertz, ambaye  ana  umri  wa  miaka  19 , Thilo Kehrer , mwenye  umri  wa  miaka  21, na Nico Shulz  mwenye  umri  wa  miaka  25.

“Uzoefu ni  msingi  muhimu  hata  kwa wanaoanza  upya,” Loew alisema. “Na  wachezaji  vijana, wenye  uchu  wanaweza  kusaidia  katika  majukumu  muhimu  mbeleni.”

Mshambuliaji  wa  pembeni Sane, ambaye  alichaguliwa  kuwa  mchezaji  bora kijana  katika  ligi  ya  England  ya  Premier League msimu  uliopita  baada  ya  kuisaidia  Manchester  City  kupata  ubingwa, Petersen na  Tah  waliondolewa  kutoka  katika  kikosi  cha  mwisho kilichoshiriki  katika  fainali  za  kombe  la  dunia  nchini  Urusi  mwezi  Juni.

Loew amemuacha  mchezaji  wa  kati Sami Khedira, aliyekuwamo  katika  kikosi  kilichoshinda  kombe  la  dunia mwaka  2014, kwa  ajili  ya  mechi za  mwezi  ujao lakini  ameendelea  kuwa  na  imani  na  wengine  kadhaa  ambao  wamecheza  chini  ya  kiwango  nchini  Urusi,  miongoni  mwa  wachezaji  17  kati  ya  23  waliokuwa  katika  kikosi  kilichokwenda Urusi.

“Umiliki  wa  mpira  katika  ligi ni  muhimu  lakini  katika  awamu  ya  mtoano  kunahaja  ya  kubadilika. Hilo  lilikuwa  kosa  langu  kubwa,” Loew  aliwaambia  waandishi  habari. “Kwamba  naamini kwa  mchezo  wa  kumiliki  mpira  tutapita  katika  awamu  ya  makundi.

“Nilitaka  kufanya  bora  zaidi, na kufanya bora  zaidi umiliki  wa  mchezo . Lakini  kila  mchezo  ni  wa  mtoano. Nilipaswa  kutambua kwamba  tunahitaji  kuchukua tahadhari  zaidi. Badala  yake  nilitaka  kuingia  katika  hatari zaidi.”

Loew  pia  amesema  alishindwa  kuwatia  hamasa  zaidi  wachezaji  wake  kwa  ajili  ya  michuano  hiyo. “Baada  ya  kushinda  mwaka 2014 na  kuwa  juu tulishindwa  mara  hii , kuwasha  moto mkubwa  ili kila  mmoja  ajihisi kuwa  na  hamasa,” Loew  alisema.

Author: Bruce Amani

Facebook Comments