Kocha wa zamani wa Liverpool aondoka hospitali baada ya kuugua Corona

Nguli wa Liverpool Sir Kenny Dalglish amepewa ruhusa rasmi leo ya kuondoka hospitalini alikokuwa amelazwa baada ya kugundulika kuwa na maambukizi ya virusi vya Corona wiki iliyopita.

Kocha na mchezaji wa zamani wa Scotland Dalglish, 69, alipelekwa hospitalini Jumatano iliyopita kwa ajili ya matibabu kufuatia kuwa na dalili za COVID-19.

Strika huyo wa zamani wa Celtics na Scotland amesema anawashukuru wote waliomtumia salamu za pole akiwa hospitalini.

“Nina furaha kubwa kurejea nyumbani kuonana na familia yangu. Mke wangu(Marina) na mimi mwenyewe tunawashukuru sana kwa salamu zenu, tunawapongeza pia NHS kwa huduma bora mliyoitoa kwangu”.

Baada ya kutolewa hospitalini Dalglish ataendelea kuwa karantini nyumbani kwake kama watalaamu ambavyo hushauri.

Dalglish alishinda mataji manne akiwa ligi ya Scotland kabla ya kuhamia Liverpool mwaka 1977 ambapo alishinda mataji nane ya ligi daraja la kwanza ambapo ndiyo ligi kuu pia aliingia kwenye rekodi baada ya kushinda kama mchezaji lakini pia kama kocha.

Aidha, anakumbukwa pia kuwa alikuwa kocha kipindi kile ambacho mashabiki 96 wa Liverpool walipoteza maisha katika ajali ya ndege mwaka 1989 walipokuwa wanaelekea kucheza nusu fainali dhidi ya Nottingham Forrest.

Mwaka 1995 alishinda EPL akiwa na Blackburn Rovers kama kocha wa timu hiyo.

Anakuwa mwanamichezo wa tatu kuugua kisha kupona COVID-19 kutoka EPL ambapo kocha Arteta na mchezaji wa Chelsea Callum Hudson-Odoi wamepona kabisa.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends