Kombe la Dunia ngazi ya klabu lapigwa kalenda mpaka mwakani 2021

Shirikisho la Soka Duniani FIFA limehamisha muda wa mashindano ya Kombe la Dunia ngazi ya vilabu mpaka Februari 2021 kutoka mwezi Disemba ambapo yalitakiwa kufanyika mwaka huu kutokana na janga la virusi vya Corona.

Wawikilishi wa bara la Ulaya wanajulikana kuwa ni Bayern Munich baada ya kushinda taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya mwezi Agosti mbele ya Paris St-Germain lakini janga la Covid-19 limeathiri baadhi ya mabara na kushindwa kutoa bingwa wa mabara husika.

Lakini licha ya kubadilika kwa muda wa kufanyika kwa mashindano hayo lakini sehemu ni ile ile Qatar kuanzia tarehe 1-11 mwezi Februari.

Anayeshikilia taji hilo ni Liverpool baada ya kushinda Disemba mwaka 2019.

Author: Asifiwe Mbembela