Kosgei ailenga Tuzo ya IAAF ya Mwanariadha Bora Mwanamke

Bingwa wa Marathon anayeshikilia rekodi ya dunia Mkenya Brigid Kosgei ni mmoja wa wanariadha watano wanaowania tuzo ya Mwanariadha Bora Mwanamke katika mwaka wa 2019.

Kosgei alivunja rekodi iliyowekwa na Muingereza Paula Radcliffe ya miaka 16, kwa kukimbia katika muda wa saa mbili, dakika 14 na sekunde nne ili kushinda mbio ya Chicago Marathon. Kosgei, mwenye umri wa miaka 25 pia ndiye mshindi mwenye umri mdogo zaidi wa mbio za London Marathon mwezi Aprili.

Mmarekani Dalilah Muhammad, Mjamaica Shelly-Ann Fraser-Pryce, Mvenezuela Yulimar Rojas na Mholazi Sifan Hassan pia wanawnia tuzo hiyo.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends