Kosgei tayari kutetea taji lake la London Marathon

Mwanariadha anayeshikilia rekodi ya ulimwengu ya mbio ya mbio za marathon kwa wanawake Mkenya Brigid Kosgei atarejea kuitetea taji lake katika mbio za mwaka huu za London marathon. Kosgei alitetea taji lake la Chicago Marathon Oktoba mwaka jana na kuivunja rekodi iliyowekwa na Muingereza Paula Radiclife iliyodumu miaka 16.

Mkenya mwenzake na ambaye anashikilia rekodi ya ulimwengu Eliud Kipchoge, ambaye alikimbia marathon chini ya masaa mawili Oktoba mwaka jana, tayari amethibitisha kuwa atalitetea taji lake la London. Wanariadha wengine watakaoshiriki ni mshindi wa London Marathon 2018 Vivian Cheruyiot, mshindi mara tatu wa Berlin Marathon Gladys Cherono na bingwa wa sasa wa ulimwengu Ruth Chepngetich.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends