Koulibaly aifungia Napoli na kuifanya Juventus kusubiri

Kalidou Koulibaly alifunga mabao yake mawili msimu huu wakati Napoli walipata ushindi wa 3 – 1 dhidi ya Chievo na kuwafanya Juventus kusubiri kwa wiki alau wiki nyingine kabla ya kubeba taji la Ligi Kuu ya Italia.

Beki huyo wa kati alifunga bao la kichwa kutokana na mkwaju wa kona uliopitwa na Dries Mertens na kuwaweka vijana hao wa Carlo Ancelotti kifua mbele na Arkadiusz Milik akasukuma wavuni kombora kutoka hatua 25. Koulibalya alifyatua shuti kali na kufunga la tatu.

Chievo wameshushwa daraja kutokana na matokeo hayo, baada ya kushinda mechi moja tu ya Serie A msimu huu, ijapokuwa Bostjan Cesar aliwafungia bao la kufutia machozi katika sekunde ya mwisho ya mchezo.

Juve, watabeba ubingwa wa nane Jumamosi ijayo kama watapata pointi moja dhidi ya Fiorentina.

Author: Bruce Amani