Kubeti kwamuingiza matatizoni Ibrahimovic wa AC Milan

267

Shirikisho la Kandanda barani Ulaya – Uefa limekusudia kufanya uchunguzi juu ya mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic kufuatia kuhusishwa na Kampuni ya kubeti.

Kwa mujibu wa ripoti ambazo zimetolewa nchini Sweden zinasema Zlatan amevunja matakwa na sheria na kuwa muwekezaji mwenza katika Kampuni moja ya kubashiri matokeo.

Ibrahimovic, 39, kuwa na ushirika huo kunavunja kanuni ya kinidhamu ya Uefa ambayo inasema mchezaji hatakiwi kufungamana na makampuni ya kubeti.

Wiki iliyopita aliingia kandarasi mpya na AC Milan ambayo itatamatika kipindi ambacho atakuwa na miaka 40, ndani ya Milan amefunga goli 17 katika mechi 25 kwenye mashindano fulani.

Author: Asifiwe Mbembela