La Liga kurejea rasmi kutimua vumbi Juni 11

Ligi Kuu nchini Hispania La Liga itaendelea tena Juni 11 baada ya kusimama kwa takribani miezi mitatu kwa sababu ya Covid-19 ambapo msimu mpya wa 2020/2021 ukikusudiwa kuanza Septemba 12.

Akizungumzia kurudi kwa ligi hiyo Rais wa ligi ya Hispania Javier Tebas amesema ‘wamejipanga vizuri’.

Hata hivyo Jumatatu iliyopita Rais huyo alisema mchezo wa ufunguzi utakuwa baina ya Real Betis na Sevilla mtanange wa watani wa jadi.

Tebas aliongeza kwa kusema wana mpango wa kujaribu kuweka sauti za mashabiki wakishangilia mechi mbalimbali ili kuleta hali ya kumfanya shabiki ajione kama yupo uwanjani pindi watakapo kuwa wanangalia michezo iliyosalia.

Wote watakao kuwa wanaangalia nyumbani watakuwa na uwezo wa kuchagua kuangalia mechi ikiwa kimya bila kelele za mashabiki au kuangalia mechi huku ikiwa na kelele mithili anaangalia mechi iliyo na mashabiki.

Siku ya Jumamosi Waziri Mkuu wa Hispania Pedro Sanchez alitoa ruhusa ya kuanza shunguli za kimichezo kuanzia Juni 8.

Wiki nane zilizopita wachezaji wa vilabu tofauti tofauti vya Li Liga walianza mazoezi ya kila mtu pekee yake kabla ya makundi madogo madogo.

Soka Hispania lilisitishwa Marchi 12 kutokana na janga la virusi vya Corona, ambapo ligi ilisimama wakati Barcelona ikiongoza ligi kwa tofauti ya alama mbili dhidi ya timu iliyonafasi ya pili Real Madrid huku mechi 11 pekee zikiwa zimesalia.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends