La Liga yatafuta uungwaji mkono wa mchuano wa Miami

Ligi ya Kuu ya kandanda Hispania imeanzisha kampeni ya kuonyesha kuwa mashabiki wa Marekani wanaunga mkono mpango wake wa kuanzisha utamaduni wa kuandaa mechi moja ya soka nchini Marekani kila msimu

La Liga na wadhamini kutoka Marekani kwa pamoja wameanza kuwaomba mashabiki kuweka saini makubaliano ya kuunga mkono mchezo wa La Liga kati ya FC Barcelona na Girona uchezwe Miami Januari mwakani.

“Katika juhudi za kuonyesha namna ambavyo wadau wanaunga mkono kupeleka mchezo Marekani, tumeanzisha maombi maalumu ya kuwahamasisha mashabiki wa soka kutoa maoni yao mtandaoni,“ Imesema taarifa ya La Liga, kampuni ya burudani ya Relevant.

Lengo la kuupeleka mchezo huo Marekani ni kukuza hadhi na kufahamika kwa ligi kuu ya Hispania ingawa juhudi hizi zimepingwa vikali na viongozi, na baadhi ya mashabiki wa soka nchini Hispania. Mgogoro huo umekuwa kati ya wadau wote ambapo kila upande umekuwa ukijitahidi kutetea hoja zake.

Katika siku za hivi karibuni FIFA ilipinga mpango huo baada ya kupokea maombi kutoka CONCACAF na mashirikisho nchini Marekani na Hispania ambayo yana haki ya kusema kama mechi hiyo ichezwe Marekani au la,pamoja na UEFA.

Ruhusa ya FIFA kukubalia mchezo huo kuchezwa Marekani sio lazima ingawa upinzani wake ulikuwa hatua ya kurudi nyuma kwa La liga.

Chama cha soka nchini Hispania kimepanga kupeleka madai yao katika mahakama ya usuluhishi michezoni kudai kukataliwa kwa kufanyika mchezo huo, ambapo pia kimesisitiza kuwa kipo tayari kwenda mahakama ya ndani ya Hispania kama shirikisho litagoma kurusu mchezo huo kuchezwa nje ya Hispania.

Endapo mchezo huo utachezwa Marekani utaongeza umaarufu wa La Liga kimataifa na kupunguza pengo baina yake na Ligi Kuu ya England inayopendwa zaidi. (AFP)

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends