Lampard akaribishwa darajani licha ya Chelsea kubanwa na Leicester

Frank Lampard amesema kuwa kocha wa Chelsea dimbani Stamford Bridge kwa mara ya kwanza ni kitu cha kutimiza ndoto zake, licha ya bao la kichwa katika kipindi cha pili lake Wilfred Ndidi kuipa Leiceter City pointi moja muhimu.

Chelsea iliongoza mchezo huo mapema kupitia shuti la ndani ya boksi la kinda Mason Mount, 20, akitumia udhaifu wa kiungo mkabaji Ndidi kisha kumchambua vyema Kasper Schmeichel.

Baada ya goli hilo chelsea ilipunguza kasi na kuanza kucheza mchezo wa pasi ndefu na za haraka kupitia kwa Pulisic na Pedro.

Walitengeneza nafasi bora kupitia kwa N’Golo Kante, na Pedro licha ya matukio yote hayo kushindwa kufanya vizuri.

Mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika Chelsea 1-0, kipindi cha pili kilianza kuwa kizuri kwa Leicester ambao waliandika goli la kusawazisha kupitia kwaNdidi aliyefunga kwa kichwa akimalizia pigo la kona la Madison. 

Matokeo ya mchezo huo yanazifanya timu zote kushindwa kupata alama tatu kwenye michezo miwili ya EPL, Chelsea ina alama moja wakati Mbweha wana pointi 2.

Mchezo mwingine wa leo umeshuhudia Crystal Palace kupoteza mchezo dhidi ya timu iliyopanda daraja msimu huu ya United goli 1-0.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends