Lampard akaribishwa Premier League kwa kipigo Old Trafford

Manchester United imeandika historia mpya kabisa ya kuibuka na ushindi mkubwa zaidi kuwai kutokea ndani ya  Old Trafford tangu mwaka 1965 ilipocheza na Chelsea kwa kushinda goli 4-0.
Hiki kinakuwa kipigo kizito zaidi kwa kocha Frank Lampard ambaye mchezo wa leo umefungua ukurasa mpya wa kazi yake ndani ya Chelsea ukiwa ni mchezo wa kwanza.
Mshambuliaji wa Manchester United Marcus Rashford alikuwa mwiba mkubwa kwa Chelsea baada ya kufunga goli mbili huku akiweka rekodi ya kufunga penati zote nne alizochukua jukumu hilo ngazi ya taifa na klabu.
Goli lingine limefungwa na Anthony Martial, ambaye amerejeshewa jezi namba tisa aliyokuwa akiivaa kwenye msimu wa kwanza kabla ya Zlatan na Lukaku kuchukua namba .
Kijana Daniel James aliingia akitokea bechi alifunga goli lake la kwanza ndani ya Manchester United dakika tisa kabla mechi kumalizika.
Kinakuwa kipigo cha 104 kizito kwa Chelsea katika ufunguzi wa mechi za Ligi Kuu ya England tangu kuanzishwa kwa klabu hiyo.
Katika mchezo huo, Manchester United ilianza na kikosi kilichomjumuisha beki ghali Harry Maguire na Wana Bissaka, huku Chelsea kukiwa na maingizo kadhaa mapya kuanzia kwa kinda Mason Mount, Tammy Abraham, na Fikayo Tomori.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends