Lampard Akubali Kuzomewa, Brentford Wavunja Rekodi ya Miaka 30

125

Kocha wa Chelsea Frank Lampard amesema anaelewa hisia za mashabiki wa klabu hiyo za kuwazomea wachezaji na viongozi wa klabu akisema ni kutokana na kutofanya vizuri kwa kipindi hiki.

Baada ya kufungwa bao 2-0 dhidi ya Brentford dimba la Stamford Bridge, Chelsea imefikisha mechi tano mfululizo bila kushinda mchezo wowote ambapo wanaifikia rekodi waliyowai kuiweka ya kutoshinda mechi kama hizo miaka 30 iliyopita.

Vipigo vyote vitano vimetokea Chelsea ikiwa chini ya lijendi na mfungaji bora wa muda wote klabuni hapo Frank Lampard, 44, aliyerudi kwa mara ya pili kama kocha April 3.

“Nadhani wanazomewa kwa sababu hatufanyi vizuri, mashabiki hapa wamezoea kushinda lakini hatupo hivyo”, alisema Lampard akizungumza na BBC.

“Sisi kama wachezaji na viongozi tupaswa kuzichukua kelele hizo katika njia chanya ya kuhakikisha tunaanza kufanya vizuri”.

Author: Bruce Amani