Lampard alia na uchovu kwa wachezaji wake baada ya Chelsea kuchapwa 2 – 1 na Wolves

251

Kocha wa Chelsea Frank Lampard amesema wachezaji wake wana uchovu kufuatia kukutana na kipigo cha goli 2-1 dhidi ya Wolves mtanange wa Ligi Kuu nchini England uliopigwa Jana Jumanne.

Bao la Pedro Neto dakika ya 95 limeinyima Chelsea hata bahati ya kuondoka na pointi moja dimbani Molineux. Daniel Podence alisawazisha bao la mshambuliaji wa Kifaransa Olivier Giroud ambaye alikitanguliza mbele kikosi cha The Blues chini ya Frank Lampard.

Kinakuwa kipigo cha pili mfululizo kwa Chelsea baada ya mechi ya juzi dhidi ya Everton kupoteza mechi hiyo kwa goli 1-0.

Author: Bruce Amani