Lazio yamnyakua Maurizio Sarri akichukua nafasi ya Inzaghi

Kocha wa zamani wa Chelsea Maurizio Sarri ameingia kwenye kandarasi ya kuinoa klabu ya Lazio inayoshiriki Ligi Kuu nchini Italia Serie A mpaka mwaka 2023.
Klabu hiyo imethibitisha Jumatano usajili wa kocha huyo kwa kuweka picha ya sigara, koti na trakisuti zikiwa ni ishara ya usajili wa kocha huyo mwenye utamaduni wa kuvuta sigara.
Mkataba wa Sarri unaelezwa kuwa utatua na jina la kiungo mshambuliaji wa England na klabu ya Chelsea Loftus Cheek ambaye kandarasi yake The Blues inamalizika mwishoni mwa mwezi Juni 2024, na alikuwa Fulham kwa mkopo.
Sarri anatua ndani ya Lazio kipindi ambacho kumekuwa na fukuza fukuza ya makocha na kutimuka, tumeshuhudia Inter Milan akiondoka Antonio Conte, Juve akitoka Andrea Pirlo na Simone Inzaghi akiondoka Lazio, huku Jose Mourinho akiingia mkataba na AS Roma.

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares