Leeds yamnyatia Daniel James wa Man United

Leeds United iko mbioni kukamilisha uhamisho wa winga mwenye kasi kutokea Manchester United Daniel James kwa dau la pauni milioni 30.

Kocha Marcelo Bielsa wa Leeds United amekuwa akivutiwa na uchezaji wa James tangia akiwa Swansea ambapo alitamani kumsajili Januari 2019 ingawa baadaye dili lake lilikomea mikononi mwa Manchester United.

Katika mechi 74, Daniel James raia wa Wales amefunga goli 9 kwa Mashetani Wekundu.

Hata hivyo, ujio wa Cristiano Ronaldo wa dau la pauni milioni 12.85 unaifanya namba ya kuanza kwa James kuwa mashakani kwa winga huyo mwenye umri wa miaka 23.

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares