Leicester City yaichakaza Manchester City 5 – 2

151

Manchester United imekutana na kipigo kizito cha goli 5-2 dhidi ya Leicester City katika mchezo wa Ligi Kuu nchini England uliopigwa dimba la Etihad Jana Jumapili. Kipigo hicho kinakuwa cha kwanza kikubwa kwa Manchester City nyumbani tangu mwaka 2013 huku strika Jamie Vardy akifunga bao tatu pekee katika goli hizo tano.

Wakati City wakipigwa, Leicester City iliyochini ya kocha Brendan Rodgers imekwea mpaka nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa EPL ikiwa ni katika raundi ya tatu. Magoli mawili ya Manchester City yamefungwa na winga wa Algeria Riyard Mahrez na beki wa pembeni ambaye ni ingizo jipya Nathan Ake.

Vardy alifunga bao lake kwa njia ya penati kabla ya kuendelea kuiadhibu Manchester City kupitia krosi ya  Timothy Castagne. Bao lingine Leicester limefungwa na kiungo wa kiingereza James Maddison ambalo linakuwa bao lake la kwanza tangu mwezi Januari 1.

Bao la mwisho liliwekwa kimiani na Youri Tielemans kwa njia ya penati lakini tayari mshambuliaji Vardy alikuwa ametoka akiwa amekwamisha mipira nyavuni mara tatu. Kikosi cha Guardiola kimepokea kipigo hicho kikubwa nyumbani na kukamata nafasi ya katikati ya msimamo wa ligi kuu nchini England.

Author: Asifiwe Mbembela