Leicester City yaiduwaza Chelsea na kubeba Kombe la FA

Kikosi cha kocha Brendan Rodgers Leicester City kimefanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Chelsea mchezo wa Kombe la FA uliopigwa dimba la Wembley Leo Jumamosi, likiwa taji la kwanza katika historia ya klabu hiyo.
Bao pekee kwenye mchezo huo limefungwa na kiungo mshambuliaji Youri Tielemans raia wa Ubeligiji aliyepiga shuti kali kunako dakika ya 63 na kuwanyima nafasi The Blues chini ya Thomas Tuchel kupata goli la kusawazisha, ingawa katika mchezo huo kulitokea utata wa video saidizi kwa waamuzi VAR baada ya baoa la Chillwell kukataliwa kuwa ameotea.
Linakuwa taji lao la kwanza tangia mwanzo wake 1969, goli ambalo liliwanyanyua mashabiki 21,000 waliojitokeza katika uwanja wa Wembley kwa mara ya pili kutokana na vizuizi vya Janga la Virusi vya Corona.
Kocha Tuchel kwa sasa nguvu kubwa atakuwa anahamishia kwenye kung’ang’ania kucheza michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao pamoja na mchezo wa fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Manchester City itakayopigwa Mei 29 nchini Ureno.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares