Leicester wabanwa mbavu na Southampton katika sare ya 1-1

Licha ya kuwa pungufu kwa zaidi ya dakika 80 kikosi cha Southampton kimefanikiwa kuwabana Leicester City katika sare ya goli 1-1, mchezo wa Ligi Kuu nchini England uliopigwa Ijumaa na kupunguza kasi ya kuwania nafasi nne za juu kucheza michuano ya Ulaya.

Jannick Vestergaard alionyeshwa kadi nyekundu kwa kumchezea rafu mshambuliaji wa kimataifa wa England Jamie Vardy baada ya dakika 10 za mchezo, rafu iliyokuwa inaelezwa kuwa imemzuia nafasi ya kufunga, Vastergaard inakuwa kadi yake ya kwanza katika mechi 200.

Mbali na kuwa pungufu, Southamption walitangulia kujipatia bao kupitia kwa James Ward-Prowse aliyefunga kwa njia ya penati baada ya mpira wa Stuart Armstrong uliokuwa unaelekea golini mwa Mbweha Leicester City kugusa mkono wa mshambuliaji Kelechi Iheanacho.

Jonny Evans alisawazisha goli hilo akimalizia kwa kichwa krosi ya Iheanacho dakika nane za kucheza, mlinda mlango wa Southamption Alex McCarthy alikuwa bora kuokoa michomo ya jamie Vardy na kuipa alama moja timu yake.

Alama moja inawapa City nafasi ya kuweka tofauti ya alama nane dhidi ya West Ham United ambao wako nafasi ya tano.

Wakati Southampton wanavuna alama moja na kuwafanya wawe salama kwa alama 10 katika eneo la kushuka daraja.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares