Desisa ashinda mbio za wanaume za New York Marathon 2018

109

Lelisa Desisa wa Ethiopia alishinda mbio za New York City Marathon 2018 kwa upande wa wanaume Jumapili kwa kutumia muda wa saa mbili, dakika tano na sekunde 59

Desisa mwenye umri wa miaka 28, alishinda taji la New York kwa mara yake ya kwanza, kwa kuwashinda Shura Kitata, mwenye umri wa miaka 22 pia kutoka Ethiopia na Geoffrey Kamworor mwenye umri wa miaka 25 wa Kenya, na ambaye ni bingwa mtetezi wa New York City Marathon.

Desisa awali alishinda Boston Marathon katika mwaka wa 2013 na 2015

Author: Bruce Amani