Lewandowski afunga hat-trick katika ushindi wa Bayern

Robert Lewandowski alifunga hat-trick wakati mabingwa wa Bundesliga Bayern Munich walipata ushindi wao wa kwanza wa msimu kwa kuwacharaza kwa urahisi Schalke 3 – 0.

Vijana hao wa kocha Niko Kovac walijibu kimtindo baada ya kuanza msimu kwa sare ya 2 – 2 dhidi ya Hertha Berlin. Mshambuliaji wa Poland Lewandowski alifunga la kwanza kwa njia ya penalty, kabla ya kuongeza mawili zaidi katika kipindi cha pili ikiwa ni hat trick yake ya tisa kwenye ligi.

Katika matokeo mengine ya Jumamosi

Mainz 1 – 3 B Mgladbach
Augsburg 1 – 1 Union Berlin
Duesseldorf 1 – 3 B Leverkusen
Paderborn 1 – 3 Freiburg
Hoffenheim 3 – 2 Werder Bremen

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends