Lewandowski aifikia rekodi ya Gerd Mueller katika Bundesliga

Mshambuliaji wa kimataifa wa Poland Robert Lewandowski ameandikisha rekodi ya kufunga magoli sawa na mshambuliaji Gerd Muller, amefikia rekodi hiyo kufuatia kufunga goli katika sare ya goli 2-2 na Freiburg mchezo uliopigwa Leo Jumamosi.
Strika huyo wa zamani wa Borussia Dortmund kwa sasa amefunga goli 40 katika mechi 28 za Ligi Kuu nchini Ujerumani Bundesliga ndani ya msimu mmoja.
Muller akiwa na umri wa miaka 49, alikuwa na wastani wa kufunga goli kila baada ya dakika 77 pale alipoandikisha rekodi hiyo mwaka 1972, lakini Lewandowski ana wastani wa dakika 58 kwenye kila goli.
Ndani ya mechi 19 alifunga goli 18 kwenye Bundesliga miongoni mwa takwimu hatari kwa mshambuliaji huyo na alishindwa kufunga goli kwenye mchezo mmoja tu dhidi ya Hertha Berlin Februari 5.
Baada ya kufunga goli hilo, Lewandowski alinyanyua fulana yake ambayo ndani kulikuwa na picha ya Gerd Muller akionyesha heshima kwa Mjerumani huyo.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares