Lewandowski aipa ushindi Bayern mbele ya Dynamo Kyiv Uefa

Robert Lewandowski ameendeleza ubora wa kuzifumania nyavu baada ya kufanikiwa kufunga goli katika mechi tisa mfululizo ambapo pia amefunga goli moja katika ushindi wa goli 2-1 walioupata Bayern Munich dhidi ya Dynamo Kyiv mchezo wa Kundi E.

Mshambuliaji huyo wa Poland, goli lake lilikuwa linatoa alama nane zaidi ya zile ambazo Barcelona wanazo kwenye kundi hilo.

Mabao ya Bayern Munich yamefungwa na Lewandowski ambaye alifunga goli la kwanza kwa tiki-taka kabla ya Kingsley Coman, kufunga goli la pili hata hivyo ungwe ya pili ilikuwa ya Dynamo ambapo Denys Harmash alifunga goli la kufutia machozi.

Licha ya ushindi huo, Bayern walikuwa wanawakosa wachezaji wachezaji muhimu kama kama Joshua Kimmich, Serge Gnabry, Jamal Musiala, Eric-Maxim Choupo-Moting na Michael Cuisance baada ya kuwa karibu na mtu ambaye alikuwa na dalili za Uviko-19.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends