Libya yachukua nafasi ya Tunisia katika CHAN 2022

Libya imekubali, ombi la Shirikisho la soka barani Afrika CAF, kushiriki fainali ya mwaka 2022 kuwania taji la CHAN, itakayofanyika nchini Cameroon mwezi Aprili.

Nchi hiyo, inachukua nafasi ya Tunisia, ambayo licha ya kufuzu ililiamua kujiondoa kwenye michuano hiyo inayowashirikisha wachezaji wanaocheza soka nyumbani.

Shirikisho la soka nchini Tunisia, lilisema lilifikia hatua hiyo, baada ya vlabu nchini husema havitawaruhusu wachezaji kwenda kushiriki katika michuano hiyo kwa kile inachosema, michuano ya CHAN haipo kwenye kalenda ya FIFA.

Kutokana na hatua hiyo, Shirikisho la soka barani Afrika, limeitiza faini ya Dola 50,000 na kuifungia Tunisia kushiriki katika michuan ya CHAN mwaka 2022.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends