Licha ya ahadi kibao, Ihefu yashuka daraja

Ng’ombe hanenepi siku ya mnada, kauli ambayo inaweza kuwa sawa na mipango ya kikosi cha Ihefu kutoka Mbeya ambacho kiliweka mipango lukuki kipindi cha mwishoni kabisa mwa Ligi badala ya kuanza mapema kabisa jambo ambalo lilifanya ng’ombe akashiba na si kunawiri na kunenepa.

 

Imeshuka daraja msimu huu baada ya kupoteza kwa kufungwa bao 1-0 na KMC kwenye mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu uliopigwa leo kwenye Dimba la Uhuru jijini Dar es Salaam.

 

Itakumbukwa ikiwa zimesalia mechi 10 kumalizika kwa VPL, uongozi wa Ihefu uliotoa ahadi kwa wachezaji kuhakikisha wanaibakisha timu kwani zawadi nono itakuwa juu yao.

 

Bao la Charles Ilamfya alilofunga dakika ya 81 limedidimiza na kupoteza jumla matumaini ya Ihefu kubaki Ligi Kuu kwa msimu ujao kwani ilihitaji ushindi ili kugombea nafasi ya kucheza mechi za mtoano lakini imeshindwa.

 

Ikiwa ni msimu wake wa kwanza kushiriki Ligi Kuu Bara, Ihefu imeshuka tena na kurudi Ligi Daraja la Kwanza baada ya kumaliza ligi ikiwa na alama chache (35) ambapo inaungana na Mwadui na timu nyingine mbili kushuka daraja moja kwa moja.

 

Mchezo huo wa Leo Jumapili ulianza kwa timu zote mbili kucheza kwa tahadhari huku vita kubwa ikionekana eneo la kiungo kwa timu zote mbili.

 

Ihefu inaungana na Mwadui Fc, pamoja na Gwambina FC ya Mwanza kushuka daraja, ingawa Gwambina na Ihefu ulikuwa msimu wa kwaza kupanda.

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares